PHOTOGRAPHY :JUSTINE KAZAURA
MODEL : MACKLINE ALEXENDER
DESIGN& RETOUCH :ADELINA TIBESIGWA
THEME: NJE vs NDANI YA STUDIO
kama mtu angeniuliza siku ya jana ilikuwaje basi sitosita kumwambia "jumapili ya jana ilikuwa ndefu!" sababu ni kwamba kwanza, tumeangaika karibia siku nzima kutafuta mahali pa kupigia picha za nje tumekuja kupapata muda umeishaenda hivyo basi tukawa tunapiga picha za harakaharaka tukikimbizana na muda asikwambie mtu picha za nje kazi! lakini tulifanikiwa kupata kile tulichikitaka ingawa picha zimekuwa chache......
leo nimeamua niwaleeteni nyinyi mringanishe kwa sababu mi nimeringanisha, nimamaliza, na nimeishapata majibu yangu sasa kazi imebaki kwako, hivi picha unazopigia ndani ya studio na nje ya studio utofauti wake ni hupi? kama jibu unalo ussite kuniambia

jana tumepiga picha za aina mbili, hivyo hivyo za ndani na nje ya studio, kwa mtazamo wangu picha tulizopigia studio zimekuwa rahisi katika upigaji wake wala siwezi kuziongelea sana, shuhuri ilikuwa kwenye kupiga picha za nje, kwanza kabisa tulichelewa kwenye eneo tulilokuwa tunapaswa kupigia picha kwa kweli kitendo hicho kilitugharimu hatukuweza kupiga picha zaidi kwa sababu ya muda na wakati nadhani umenielewa hapo, picha za nje zinahitaji umakini wa hali ya juu! sichoki kusema hivyo
kwa picha zaidi unaweza kuangalia kwenye gallery au kuangalia facebookpage yetu https://www.facebook.com/pages/Light-photo-studio/136259433243570 kwa hayo basi napenda kusema siku njema! paka wakati mwingine................enjoy!