LANDSCAPE PHOTOGRAPHY

PHOTOGRAPHY : JUSTINE KAZAURA

DESIGN & RETOUCH : ADELINA TIBESIGWA

LOCATION : MIKOCHENI (outdoor photography)

LANDSCAPE PHOTOGRAPHY
Kwanza kabisa napenda kuanza kwa kusema, samahani nimejaribu kutafuta neno la kiswahili kwa ajiri ya mada hii nimekosa,ili nyinyi mwelewe ni ujumbe gani mnataka niwafikishie ndo nikaona bora nilete hivi hivi kwa lugha ya kingereza.... isitoshe kisawahili ni kigumu ila najitahidi hivyo hivyo

Landscape photography ni picha ambazo zinapigwa zikiwa na makusudio ya kuonesha mazingira ya aina yoyote ile yanaweza kuwa mazingira ya baharini, msituni,  jua likiwa linachomoza au kuzama, nakadharika zote hizo zinapigwa kwa lengo moja tu kukufanya utambue ni uzuri gani wa mazingira ulio kuzunguka!

kuna sehemu na maeneo mazuri sana ambayo yakipigwa picha aisee! we mwenyewe unakubari, sawa! picha nyingi zinapigwa zikiwa na lengo la kugusa hisia zetu, lakini Landscape photography imepita zote (hiyo ni kwa mtazamo wangu),


pia kuna maeneo ambayo watu wengi hawajafika na wala hawategemei kufika, hapo ndipo humuhimu wa landscape kwa mpiga picha unapoonekana, tazama hiyo picha hapo juu, imepigwa hapahapa dar es salaam, maeneo ya mikocheni, najuaa sio wote ambao wameishafika Mikocheni lakini kwa kuangalia jinsi ilivyopigwa inakuletea hisia fulani na maswali mengi labda. unajiuliza "hapa ni wapi?  alafu labda ukajijibu "natamani nipajue" au "nitenda siku moja kupaangalia" hizo ndizo nguvu ya landscape photography! ina uwezo mkubwa wa kubadilisha mtazamo wako, kwa habari zaidi unaweza kutufata kwenye ukurasa wetu wa facebook https://www.facebook.com/pages/Light-photo-studio/136259433243570
zaidi na hayo naweza kukutakia weekendnjema!