PICHA ZA "ACTION"

PHOTOGRAPHY :JUSTINE KAZAURA

MODEL: SASHA SETH

DESIGN & RETOUCH : ADELINA TIBESIGWA


THEME : PICHA ZA "ACTION"

Kwanza kabisa "action" ni kitendo, hivyo ndivyo baadhi yetu tunavyojua na wengine wanaweza wakafafanua kwa kusema ni mwendelezo wa hatua, wengi wetu tunapenda kulitumia kama neno au msemo mahali popote pale tunapoona linahitajika

sasa leo kutoka studioni kwetu tumeamua tulitumie hili neno  na tulifanyie kazi kabisa! 
"ACTION" ndo habari ya wiki hii ntafanya kazi ya kuonesha picha za "action!" tu!na wala sio nyingine! isitoshe ndio photoshoot tuliyoifanya jumapili hii ! ilikuwa ngumu kiasi, ila tumejitahidi kufikia hapa tulipofikia hadi ukaziona picha zetu leo hii!


Ninapoingelea "action" katika picha, au picha za action, na maanisha ni jinsi gani mtu au mpigwa picha anavyo kuwa kapozi, wengi wetu tunapoenda kupiga picha huwa tunapenda kusimama au kukaa, isitoshe wengi wa kina dada hupenda pozi la kujishika kiunoni na kupindisha shingo lao kidogo! kama ni mwanaume basi huyo ndo atasimama wima au atasimamia upande, sisemi kwamba hizo ni pozi mbaya ila ni kama zinaanza kupitwa na wakati hivi!? tubadlishe angalau


Huwezi kusema umeshinda mtihani wako au umehitimu elimu yako iliyo kuwa ikikuendesha na kukuchanganya mwaka mzima ukaenda kupiga picha umesimama ukitabasau au umekaa kwenye kiti umeshika cheti chako ni kumbu kumbu sawa, lakini haitokuwa yenye nguvu kama ambayo ulipiga picha unaruka kwa furaha au ukipeana mikono na rafiki zako kwa furaha au kitendo chochote kile kinachoashiria furaha na picha za aina hiyo ndo  zinaonesha uhai! hata hukimaliza miaka kumi ukaja kuingalia tena hautoichoka kama smbayo umepiga umekaa kwenye kiti ukiwa "serious!"

picha za action pia haimanishi ni kuruka tu! najua baadhi wannahisi na kukariri hivyo, lakini kwa mtazamo wangu ni picha yoyote inayoonesha kitendo chochote unachofanya kwa wakati huo, na pia sana sana kwa jinsi ninavyoona picha nyingi za action zimeegemea kwenye matangazo! kama huamini utakapo pita mjini kwako jaribu kuangalia mabango ya matangazo ya barabarani asilimia kubwa ni  picha za "action" lakini hicho sio kigezo cha kusema watu wengine tusipige picha za action! La asha! picha unapiga kama kawaida ni kutokana na matumizi yako
 kwa picha nyinginezo tazama kwenye gallery yetu au unaweza kutembelea facebook  page yetu
https://www.facebook.com/pages/Light-photo-studio/136259433243570
 kwa leo ndo hayo! kwa hiyo kaa tayari au wengine wanasema kaa mkao wa kura kwa picha nyingi za "action" kwa hali tofauti tofauti! 
mpaka siku ijayo nakutakia "siku njema"
usishau kungalia gallery