SEHEMU YA NYUMA YA PICHA "BACKGROUND"

PHOTOGRAPHY :JUSTINE KAZAURA

DESIGN &RETOUCH COMPOSED by ADELINA TIBESIGWA


THEME: SEHEMU YA NYUMA YA PICHA
baada ya kuwekewa background
unajua muda mrefu nimekuwa nikiangaalia picha mbalimbali za aina tofauti tofauti na nimejifunza mambo mengi kutokana na picha hizo sana sana tunapokuja katika swala zima la "background" au sehemu ya nyuma ya picha...... baadhi uamua kwenda eneo husika ambapo anategemea kumuweka mlengwa wake na baadhi kama sisi tunarahisisha kazi tunampiga picha mlengwa wetu ndani ya studio alafu tunakuja kumuamishia kwenye aina yoyote ya background anayoitaka! na hicho ndicho ninacho zungumzia leo 

Katika swala zima la background inabidi huwe makini yani uwe umeisha kubuhu katika swala zima la picha ili usije ukaharibu kazi zako! kwani ni kazi inayoitaji ubunifu na akili! hiyo ni kwa mtazamo wangu sasa sijui wewe unasemaje unakaribishwa kuacha maoni kwenye chatbox yetu
Mambo ambayo inabidi uzingatie pale unapotaka kumbadilishia mteja wako background ni machache lakini ndo inakubidi huyazingatie! kwanza kabisa jua ni background gani utatumia kabla ya kumpiga picha mteja wako, pili angalia wakati gani ulikuwa ulipokuwa unapiga background yako, kwa ufupi naweza kusema angalia muda na wakati wa background yako kabla ya kuongeza picha nyingine!