MIMI NI NANI (Uzuri)

MIMI NI NANI?

Hili ni swali ambalo nina uhakika kila mtu anajiuliza katika hatua tofauti tofauti anazopitia katika maisha yake na "Uzuri" ni kitu kimoja wapo ambacho ulishawahi kujiuliza kutokana na jamii inayokuzunguka.

Kwanza kabisa ambacho inabidi ujue na utambue ni kwamba kila mtu ni mzuri, Uzuri unazaliwa nao, uzuri utoka ndani yako na kupokelewa nje na jamii inayokuzunguka na ndipo hapo uzuri wako unakamilika yaani uzuri wa ndani na nje. Mambo unayobidi uyafanye ili Uzuri wako uweze kutambuliaka ni kama haya yafuatayo

1. JALI UZURI WAKO
    Utambue Uzuri wako nakuweza kuulinda,hakikisha unatuliza uzuri wako katika mambo             unayofanya,kama akili haijatulia hata uweke nini usoni uzuri wako hautaweza kupenya na
kuonekana.


2. MAZOEZI
Fanya mazoezi na kupumzika kwa wakati bila kusahau kula kwa vipimo na kwa muda maalumu.


3.MEDITATION ( kurudia mzunguko)
 Rudia mzunguko wako wa maisha na kurekebisha pale ulipokosea au ambapo unakosea kwa kutumia  roho yako ya ndani


4. USAFI WA MWILI
    Kuwa msafi wa ndani na nje hasa hasa usafi wa mwili wako kiujumla pua, kinywa, masikio, macho hizo ni baadhi ya sehemu  lakini hakikisha pande saba za mwili wako ni safi na salama.


5. KUIGA
Hakikisha unakuwa makini na mambo unayokutana nayo usipende kuiga iga vitu wafanyavyo wenzako pasipo kutambua  maumbile yao au madhumuni yao, kila mtu ana Uzuri wake na sababu zake nawe pia ni jukumu lako kutambua sababu za uzuri wako.


6. JITAMBUE
Kila unapo jitambua na kujua wewe ni mrembo ndipo majibu hutoka wa watu au jamii inayokuzunguka wao watahukumu kupitia na jinsi unavyofikiri, unavyoongea na tabia zako kwa ujumla.

Kwa ujumla  Uzuri upo katika akili yako, kuwa na mtizamo mzuri, fikiri kutoka ndani na yo pia matendo huwa mzauri.

IMEANDALIWA NA:SAADA SEIF: