AINA ZA RANGI ZA LIPSTICK

SAADA SEIF anasema

UTUMIAJI WA LIPSTICK
Wiki hii ndani ya saluni ya Saada ambayo inapatikana Mikocheni, Saada mwenyewe anaongelea jinsi lipstick inavyoweza kutumika kwa watu wa aina mbalimbali nao wakapendeza ili mradi tu utambue ni aina gani ya rangi ya ngozi yako uliyo nayo.


Kwanza kabisa watu tunatofautiana kwa rangi zetu tulizonazo, hivyo basi mtu mwenye rangi Samawati anaweza kutumia au kupaka rangi zifuatazo ambazo ni nyekundu, mawaridi au pink, kahawia au brown na hudhurungi au maroon hizi rangi zote unaweza tumia mtu mwenye aina hiyoo ya ngozi ya Samawati na bado ukatoka bomba.

Pia kwa mtu mwenye rangi ya ngozi nyeupe ana uwezo wa kutumia rangi hizo hizo na bado akapendeza na kuvutia zaidi

Usisahau maumbile yako ya mdomo na  pia matumizi ya rangi utakayotumia au utakayo paka kwa wakati huo, yaitajika kuwa mwangalifu.

IMEANDALIWA NA
SAADA SEIF