MODELS

Photography: Justine kazaura
Models : light studio models agency
Design & retouch : Adelina Tibesigwa

MODELS

Napenda ma models  kila sekta zao ukiaanzia kwa mionekano yao, jinsi wanavyo tembea, staili zo za maisha na nichokipendeza zaidi ni jinsi wanavyoweza kutumia viungo vyao vya mwili pamoja na hisia za miili yao ili kuweza kukufikishia wewe ujumbe! hakika ni kipaji kwani sio wote wanaoweza kufanya hivyo .

Nimeanza na kujieleza bila shaka utakuwa unaelewa nini kilikuwa kinanichukulia muda wangu na kukaa kimya kwenye blog yetu, nimekuwa ninapenda picha na nimekuwa nina penda zaidi kuzi edit (graphics design) hivyo ni vitu vnavyofanya maisha yangu nione yanakamilika....... lakini mwanzo tulikuwa tunapata vikwazo vingi katika kupata watu au models wa kupiga picha jambo hili limetusumbua sana mimi na Justine lakini tunamshukuru Mungu kwa kutupatia ufumbuzi! kwa sababu mpaka sasa hivi tumefungua agency ya models ( warembo) na  wana webisite yao! hii hapa http://lightstudio6.wix.com/lsmodelagency

Light studio model agency  ndio jina tuna dili na models wa aina yote hasa hasa fashion models hilo nlikuwa sijalisema "ninapenda fashion" nayo imechangia  tuwe na model agency ambao nickname yao nawaita "Angels of light" ni wachache ila natumaini watakuwa wengi siku za mbeleni make nina amini kila kitu kinaenda kwa mipango, sio siri ninawapenda models wangu ingawa niwachanga ila ni moja ya watu wanao nipa matumaini katiaka kazi yangu hivyo kwa nguvu na kadri ya uwezo wetu kuwafikisha kweye ndoto zao.... hiyo ni ahadi.

Mpaka sasa hivi models tulio nao ni wa nne (4) ambao ni Happiness Maira, Agnes Simon, Amina Athumani na Gladnes Magnus werembo hawa wana uwezo wa kutosha hivyo ni kazi kwetu kuwafikisha pale wanapotakiwa kufika!  huku katika njia ya kushughulika na changamoto tunazo kutana nazo  lakini bado na enjoy kuona picha zao na kuzifanyia maujanja  ili aweze kufikisha ujumbe ujumbe! kwa kuona picha zo zaidi tembelea webisite yao  hapa http://lightstudio6.wix.com/lsmodelagency  na pia facebook page yao https://www.facebook.com/Lsmodelagency


Kwa hiyo kimya changu kisikuchanganye sana na kubaki na maswali mengi! kwa kazi zngu zaidi utanikuta kwenye hii website http://lightstudio6.wix.com/lsmodelagency  zaidi ya hapo nakutakia kazi njema! usikate tamaa kwenye ndoto zako hata siku moja endelea kujituma lazima ufikie pale unapotaka ukifata hivyo!