NJE vs NDANI YA STUDIO

PHOTOGRAPHY :JUSTINE KAZAURA

MODEL : MACKLINE ALEXENDER

DESIGN& RETOUCH :ADELINA TIBESIGWA

THEME: NJE vs NDANI  YA STUDIO

kama mtu angeniuliza siku ya jana ilikuwaje basi sitosita kumwambia  "jumapili ya jana ilikuwa ndefu!" sababu ni kwamba kwanza, tumeangaika karibia siku nzima kutafuta mahali pa kupigia picha za nje tumekuja kupapata muda umeishaenda hivyo basi  tukawa tunapiga picha za harakaharaka tukikimbizana na muda asikwambie mtu picha za nje kazi! lakini tulifanikiwa kupata kile tulichikitaka ingawa picha zimekuwa chache......


leo nimeamua niwaleeteni nyinyi mringanishe kwa sababu mi nimeringanisha, nimamaliza, na nimeishapata majibu yangu sasa kazi imebaki kwako, hivi picha unazopigia ndani ya studio na nje ya studio utofauti wake ni hupi? kama jibu unalo ussite kuniambia
  
mimi tayari jibu langu ninalo! picha zinazopigwa ndani ya studio ni rahisi tunapokuja katika swala zima la gharama make huangaiki sana wala kuumiza kichwa, mahitaj yake ni rahisi haungalii ni muda gani upige picha we unachofanya ni kupima mwanga wa picha zako kutokana na matumizi yako! hazina mambo mengi! sasa tukija kwenye picha za nje  ya studio nazenyewe naweza kusema hazina mahitaji mengi ila tu huwe na vifaa vya kutosha kulingana na matumizi ya picha zako unazo zitaka, kama unapenda kupiga picha za aina hizi mapendekezo yangu ni kwamba inabidi huwe makini katika swala  zima la muda na wakati, bila hivyo huwezi kupata matokeo mazuri ya picha zako! picha za nje zinahitaji maandalizi ya hali  ya juu....


jana tumepiga picha za aina mbili, hivyo hivyo za ndani na  nje ya studio, kwa mtazamo wangu picha tulizopigia studio zimekuwa rahisi katika upigaji wake wala siwezi kuziongelea sana, shuhuri ilikuwa kwenye kupiga picha za nje, kwanza kabisa tulichelewa kwenye eneo tulilokuwa tunapaswa kupigia picha kwa kweli kitendo hicho kilitugharimu hatukuweza kupiga picha zaidi kwa sababu ya muda na wakati nadhani umenielewa hapo, picha za nje zinahitaji umakini wa hali ya juu! sichoki kusema hivyokwa picha zaidi unaweza kuangalia kwenye gallery au kuangalia facebookpage yetu https://www.facebook.com/pages/Light-photo-studio/136259433243570 kwa hayo basi napenda kusema siku njema! paka wakati mwingine................enjoy!